Habari wana Hub!
Natumaini mnaendelea vizuri na karibuni katika chapisho hili ambalo leo nimeamua kukushushia jambo linalogusia hasa jinsi uhusiano ulivyo na nguvu katika mafanikio.
Chapisho hili limedhaminiwa na Detha Dagaa. Jipatie dagaa safi kabisa waliokaangwa kutoka jijini Mwanza na utafikiwa popote ulipo. Weka oda yako kwa kubonyeza WhatsApp , au kwa kupiga simu kupitia 0752 232 599.
Naam, Uhusiano unaweza kusafisha Nyota au kuua nyota yako depends ni nani unakutana naye, kwa sababu uhusiano ni baraka.
Unaweza ukawa katika uhusiano na Mwanamke/Mwanaume hata kimazungumzo/kimaelewano na kila jambo ulifanyalo hunyooka vema.
Lakini unaweza kuwa katika uhusiano na Mwanamke/Mwanaume hata kimazungumzo/kimaelewano na kila jambo ulifanyalo ni mikosi/gundu hasara na mambo kuvurugika.
Trust, spiritually tunapaswa kumuomba Mungu atuletee watu aliotupangia kuwa nao katika maisha because now days ni kama cross multiplication, maisha ya kujiegesha tu ili mradi siku ziende ndio maana tunaendelea kuwa masikini na maisha ya kubangaiza. Others tend to tell themselves kuwa nikiwa na mtu fulani sababu yeye yuko vizuri au sababu anaweza akanipa huduma ninayoitaka baasi nitaishi kwa raha.
Ndio maana siku hizi mahusiano/ndoa hazidumu, inafungwa just a week inavunjika kwa sababu pengine mtu anakuwa hayuko mahali sahihi ambapo hakupangiwa kuwa pale.
Ngoja nikupe mfano:
Kuna mwanamke aliolewa na mkwasi, awali mambo yalikuwa vizuri tu, ila baada ya miezi mitatu kila kitu kilianza kuvurugika.
Mali ilianza kuisha, upendo uliisha, kipigo na manyanyaso vikaanza kwa yule mwanamke. Aliishi maisha ya kuteseka sana hadi urembo na sura aliyojaaliwa vilipotea na alichakaa sana.
Ndoa ile ilidumu kwa takribani miaka miwili tu na baadaye waliachana ambapo walibahatika kupata mtoto.
Walipoachana kila mtu alifuata maisha yake.
Yule mwanamke alikaa kama mwaka mmoja hivi na miezi kadhaa baadae akapata mwanaume ambaye hata mahali hakumtolea. Walivyokutana tu katika harakati za maisha, wakapendana na wakaamua kuishi pamoja.
Mwanaume alikuwa na kazi ya kuuza mapanki (Samaki waliotolewa minofu/Mabaki ya Vichwa vya samaki vilivyobanikwa) na kwenda kuuza sokoni.
Yule mwanaume alianza kufanikiwa katika biashara yake na mtaji ukawa mkubwa. Baada ya hapo alifungua biashara nyingine kubwa kutokana na mtaji aliokuwa amepata ambapo alianza biashara ya bidhaa ya mafuta kuyatoa Zanzibar kupeleka mikoani.
Kiukweli mambo yao yakaendelea kuwanyookea na mwanamke akafunguliwa duka la Urembo sababu alikuwa anapenda sana mambo ya urembo.
Wakazidi kubarikiwa, wakanunua usafiri, nyumba maana awali walikuwa wamepanga. Wakajaaliwa watoto na amani ikawatawalia kwenye familia yao, hadi sasa wanaishi pamoja na mwanamke ukimtazama kama vile asiyewahi kupitia magumu. Ameng'ara ng'ari ng'ari na urembo wake wote umemrejea!
Yule mwanaume wa awali naye alipata mke mwingine na maisha yao yananaendelea vizuri tu, amani na upendo vimo ndani yao pia.
Kwahiyo basi, katika mfano huu tunaweza kusema kuwa kunauhusiano unaweza kuwa na changamoto kwa sababu watu wale walio katika uhusiano ule hawakufanywa wawe pamoja. Maisha haya ya mahusiano hatuna budi kumuomba Mungu atupe uhusiano ambao ni sahihi na ambao ametupangia yeye mwenyewe na atuepushe na hii cross multiplication yaani 'Huyu anaenda kwa asiye na asiye naye anaenda kwa huyu'.
Na kama ni Mwanamke/Mwanaume unapitia changamoto katika uhusiano wako, omba Mungu akuvushe vema kule uendako ufike salama maana bado uko kwenye safari, sababu kilichotumwa na Mungu ni kimetumwa hakina kona kona, japo kuna uhusiano awali huwa ni mgumu na baadaye huwa sawa. Lakini macho yako ya rohoni yanaweza kuona risk ya huo uhusiano.
Mimi naishia hapo siku ya leo, ila wakati ujao nitazungumzia 'UHUSIANO THABITI'.
Hakikisha tu unanifuata katika mitandao ya kijamii kupitia @deoperacc nitakuwa natoa updates kule.
Ingia tu sehemu ya kuserch kisha andika 'De Opera' au 'deoperacc' kwenye Facebook, Twitter au Instagram.
Pia, picha hiyo hapo juu haihusiani na chapisho hili.
Ahsanteni!






