Asante kwa kutembelea DoHub! 😊

Ikiwa umewahi kuguswa na kile tunachokifanya, tunakukaribisha kwa upole kabisa kuunga mkono jitihada zetu iwe kwa kuchangia kiasi chochote au hata kutangaza biashara yako kupitia jukwaa hili.

NAMNA YA KUJITOA KWA WATU SAHIHI (A true selfless sacrifice)

Siraj Kingi
0


Uhali gani mpenzi wa DoHub, karibu tena kwenye blog hii ambayo hukupa milisho mbalimbali inayoweza kukuongezea thamani na uelewa katika maisha yako. Ninathamini sana uwepo wako katika blog hii ya DoHub na ninahakikisha nakupatia kile kilichosahihi kabisa. Sapoti yako ni muhimu sana hasa katika kuendesha jukwaa hili. Iwapo utaguswa, unaweza kunishika mkono kwa namna yoyote ikiwa ni pamoja na kutangaza biashara yako kupitia jukwaa hili, au Bonyeza hapa kuchangia kiasi chochote ambacho kinaweza kunibariki nawe utabarikiwa pia. 

Leo kwenye DoHub nitazungumza kuhusu kujitoa kwa watu ambao hawaoni thamani ya kile ambacho unawapatia. 

Mwenye njaa hawezi kukaa ndani, hata akizuiwa lazima atatoka tu. Akitaka kutoka akaambiwa rudi ndani, lazima atauliza 'mpaka muda gani'? 'Nitatoka saa ngapi?', 'Mi sijazoea kukaa ndani' na mara nyingi utamkuta yupo dirishani anachungulia nje. Kama hawezi kulifikia dirisha, basi yeye hukaa mlangoni akisikiliza kama kuna mtu anakuja kufungua na hapo ukienda kufungua mlango ghafla, atapata umemng'oa kucha.

Hii inatufunza nini?

kuna baadhi ya watu wakiwa na nia huwa hawana subira, na mara nyingi huonekana wasumbufu na ndio hufanikiwa. Unaweza ukaminya mwisho wa siku utakubaliana.

Watu wengi wenye mipango thabiti, huwapima watu kwa nia na uwajibikaji.Hii ni kama kumpa au kumuahidi chakula aliyeshiba. Hawezi kuona kinachelewa, hata ukimuambia atakula wakati mwingine, yupo tayari kusubiri. Hawezi kukusumbua. Unaweza dhani ni mtulivu, la hasha! hakuna utulivu penye njaa. Kwa hiyo kama ni mtu mwenye malengo huangalia mwenye njaa kwa sababu huyo atakuwa na moyo wa kupambana na mwenye kuleta mipango mipya njinsi ya kuidhibiti njaa.

Mazingira halisi katika kujitoa kwa watu.

Kuna muda unajitoa kwa watu ambao hawaoni umuhimu wa kile unachowapa. Kiufupi niseme kwamba, "Bahati huwaangukia wasio bahati" au "Wanaoogeshwa ni wasioenda mjini".

Kuna wakati mioyo yetu hutamani kuwabeba na kuwainua watu kupitia mambo au jambo fulani eitha kwa faida au kutengeneza icon au chain ya kile kitu unachokifanya au ulichojaaliwa na mwenyezi Mungu. Lakini kujitoa huko na juhudi zote huangukia pua kwa upotevu wa muda na pengine ukajikuta uko frustrated kwa mzio hasi.

Siri ya kuvuka katika hili, ili upate watu ambao ni dhahiri.

  • Usimfuate mtu na kumweleza moja kwa moja au kumpa ushauri juu ya kile unachoona anaweza kukifanya. Kupitia njia hii, 5% ya watu sahihi ndio hupatikana. [Hapa ni sawa na kutupa ndoano kisimani ukitaraji kuvua papa].
  • Ngojea mtu mwenyewe aje akueleze hitaji na nia yake juu ya kile ambacho pengine unacho au kikiwaza kwa namna fulani. Hapa utapata watu ambao 99% wanamaanisha. Yaani kama ni biashara, muache aje mwenyewe kuomba kazi. Ataifanya kazi yako kwa ueledi na umakini.

Usimfuate mtu na kuanza kujieleza ukimbembeleza na kumpa sifa. Huyu atafanya kazi kwa kiburi na kujisikia. Hii ni kwa sababu hakuwa na nia.

Hii ina-apply katika maeneo yote kwamba, unapomshawishi mtu au kumuhitaji mtu kwa ajili ya jambo fulani bila yeye kuamua au kuwa na nia, ni ngumu sana kulithamini jambo hilo. Hata kama ukiiona mtu anajua sana, usitumie nguvu na muda kumshawishi, muache na kujua kwake.

Ni heri kukomaa na yule mtu asiyejua ila ni mwenye nia. Huyu mtafika mbali kwa sababu, kadiri mtavoendelea huongeza maarifa na huja kujua zaidi ya yule ambaye uliona anajua.

Katika fungu lingine ni kwa watu ambao hawaoni wala kujua na kuelewa uadimu na thamani ya kile ambacho umewafanyia au kuwapa.

Unaweza kuona kuwa kuna mtu ana talent au anamzunguko wa display kubwa ambapo mnaweza kufanya jambo likainuka na ukayaona matunda ya kile unachokifanya.

Unaweza kumfanyia mtu kazi kwa kujitoa na hata kumbeba ukitarajia huko aendako ataitangaza kazi yako na atakuletea watu zaidi. Hii ni nzuri hasa pale ukikutana na watu sahihi.

Ni hasara pale ukijitoa kwa mtu ambaye;

1. Hakithamini au haoni afanye nini juu ya kile ulichompatia au unachompatia. Hana malengo au hakina faida, hakitegemeeki(Hana cha kupoteza). Hii ni sawa na fundi cherehani kujitoa kumshonea mtu nguo ukitarajia huko aendako atakutangaza kulingana na display kubwa aliyonayo. Basi, yeye hufurahika na kuwa na nguo nyingi tu ndani pasipo kuzivaa. Hapa tayari unakuwa umepoteza ubunifu na muda.

2. Mtu mbinafsi. Watu wa namna hii unaweza wekeza muda na kujitoa kwa ajili yao ili nao wakutangaze na kionekane ulichomfanyia.

Lakini kwa hapa huwa tofauti, mara nyingi huwaficha watu wanaotaka na kuuliza hii product nani kafanya na imefanyika wapi. Wao hufanya hivo wakihofia kupoteza nafasi au favor wanayopata kutoka kwako. Na muda mwingine huwa-direct wale watu wanaowauliza mahali pengine. Hapa unapoteza muda na juhudi.

Mimi naishia hapa siku hii ya leo. Ninakushukuru sana kwa kuendelea kutembelea jukwaa hili la DoHub.

Unaweza kunifuata katika mitandao ya kijamii kupitia De Opera /@deoperacc

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Tafadhali Usitume Barua Taka Hapa. Maoni yote yanakaguliwa na Msimamizi.
Post a Comment (0)
 
 
Tovuti yetu hutumia vidakuzi kuboresha matumizi yako. Jifunze Zaidi
Accept !