Asante kwa kutembelea DoHub! 😊

Ikiwa umewahi kuguswa na kile tunachokifanya, tunakukaribisha kwa upole kabisa kuunga mkono jitihada zetu iwe kwa kuchangia kiasi chochote au hata kutangaza biashara yako kupitia jukwaa hili.

FAIDA YA KUISHI NA MFANYAKAZI KAMA RAFIKI/MTU WA KARIBU

Siraj Kingi
0

Habari za leo mpwa wangu? Natumaini unaendelea vizuri na karibu tena kwenye jukwaa letu la De Opera Hub. Leo nitazungumza kuhusu kuishi na mtu hasa mfanyakazi awe ni House maid au office worker. Japo hata kwa mtu wa kawaida naye itamgusa pia.

Kuna watu huwa wanalalamika juu ya kutendewa vibaya na wafanyakazi wao, kama vile kutelekezwa(Kutorokwa), na kuibiwa ama hata kufanyiwa jambo baya. Katika tafiti zangu na nilichokiona ni kwamba bosi wengi hawana care nzuri kwa wafanyakazi.

Ukitaka uishi vizuri na mtu/mfanyakazi chakwanza futa dhana ya kumuita, kumchukulia au kumtambulisha kwa watu kuwa 'Huyu ni mfanyakazi wangu', utamfanya awe perfect na afanye kila kitu kwa roho moja. Huwezi kutendewa au kufanyiwa ubaya naye abaki akitabasamu. Usiishi naye kama yeye ni adui yako. Mjali hata kwa kile asichokuomba kutoka kinywani mwake. Fikiria kuwa kuna muda anahitaji kitu fulani kama wewe ambavyo kunawakati unahitaji kitu fulani. Mjali kwa matumizi madogo madogo, usingojee apate mshahara tena kwa masimango ile hali ni haki yake. 

Faida ya kuishi na mtu/mfanyakazi kama mtu wako wa karibu/rafiki.

1. Hawezi kukuibia

Kuna baadhi ya watu hulalamika na kuwalaumu watu/wafanyakazi kuwa ni wadokozi, wanaficha pesa. 

Niseme tu kuwa mazingira kama haya yanatengenezwa na bosi mwenyewe. Ndio, kuna baadhi ya wafanyakazi ni tabia yao ila kwa asilimia 2% tu. Wengi ni wale wanaojitafutia maisha tu wala hawana makuu.

Kama ulivo wewe kuna muda unahitaji vocha, kuvaa upendeze hata yeye anahitaji pia. Mjali tu hutosikia anaficha pesa au kukuibia.

2. Hawezi kuwa kibaraka wa watesi wako.

Muda wote kumbuka, unapokuwa unaishi na mfanyakazi kwa asilimia 80% anafahamu mambo yako na maisha yako ya siri. Tabia zako anafahamu vizuri tu.

Sasa kama kuna watu wabaya/adui wanaweza kukudhuru  au kuharibu mambo yako kupitia yeye, lakini kama unaishi naye vizuri, aah! utajuzwa kila kinachoendelea.

3. Atathamini na kujali vitu kama vyakwake.

Kiukweli kama unataka vitu vyako viwe katika mikono salama, basi kitu cha muhimu ni kuishi na mfanyakazi kama rafiki wa karibu sana. Atatunza na kujali kila chochote chako.

4. Ni ngumu kufanya ukatili dhidi ya watu wako

Unapoishi na mfanyakazi kama mko vitani naye hutengeneza spiritual reply attacks sasa hii ni mbaya sana kwa sababu itaathiri ikiwa ni sanjari na kufanya ukatili kwa watoto au hata wageni wanaokutembelea.

Fikiria wewe unaondoka nyumbani unamuacha na wanao, unadhani atamakinika nao? Kila jambo atakalokuwa akilifanya, atalifanya kwa kisasi.


Wapwa, ni machache tu leo nimekuletea na niishie hapo. Ila kumbuka kupiga stori za hapa na pale. Jaribu kumueleza hata huwa unajihisije juu yake (simaanishi kimapenzi).

Mfano, unaweza msifu tu kwa kile anachokifanya ili naye ajisikie kuwa yuko sawa, hajakosea. Usikae tu kimya atashindwa kujiamini na kujiuliza kichwani mwake kuwa je anachofanya ni sahihi kweli?.

Mimi nakutakia siku njema.

Usiache kunifuata katika mitandao ya kijamii kupitia Facebook @deoperacc, Twitter (X)

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Tafadhali Usitume Barua Taka Hapa. Maoni yote yanakaguliwa na Msimamizi.
Post a Comment (0)
 
 
Tovuti yetu hutumia vidakuzi kuboresha matumizi yako. Jifunze Zaidi
Accept !