Habari za siku mpwa wangu? Natumaini unaendelea vizuri na karibu tena kwenye jukwaa letu la De Opera Hub na leo nitazungumza kuhusu Kujitambua kwa lugha ya mtaa tunasema 'Kujiongeza au kujishtukia'.
Chapisho hili limeletwa kwenu kwa udhamini mkubwa kutoka kwa ANGEL CLASSIC WEAR. Jipatie nguo kali za akina mama na akina dada kwa bei rafiki kabisa. Nguo zipo on trending fashions. Angel Classic Wear, wanapatikana Nyerere Road, Makoroboi jirani na Dunia ya Warembo jijini Mwanza. Kwa wale walio mikoa mingine, wasihofu kwa vile watafikiwa palepale walipo.
Kwa mawasiliano piga simu namba:
+255 622 601 361 au bonyeza WhatsApp
Kiukweli, kuishi kwingi ni kuona mengi na mengi hayo tuyaonayo tunayafanyia nini na tunajifunza nini? Hakika, hatuna budi kujifunza. Yaliyo mema tuyabebe na yaliyomabaya tuyaache.
Nikizungumzia kujitambua, nagusia hasa uwezo wa kuelewa na kuchukuwa hatau/maamuzi juu ya kitu au jambo fulani.
Acha niende kwenye pointi. Kuna baadhi ya watu hawajitambui kweli yaani wapo wapo tu. Si katika majukumu au mambo mengine. Siwezi kugusia kwa wa watoto kwa sababu wao ubongo wao bado unaendelea kupanuka japo kuna watoto ambao tayari wamepewa uwezo huo toka wamezaliwa. Japo mtoto umleavyo ndivyo akuavyo.
Haya sasa, kuna sisi watu wazima. Ndio maana utasikia mtu anashout 'Mtu mzima hovyo'. Yaani kwa maana ya kwamba, ni mtu mzima wa umri ila mambo anayoyafanya ni ya kijinga.
Siku zote mtu asiyejitambua, huwa anazua tafurani kwa yale anayoyazungumza au kuyatenda.
Mfano baasi, kwa wale wenye wafanyakazi. Unakuta yeye kila jambo ni hadi umuelekeze, ambavyo inakufanya uwe mtu wa kuzungumza kila wakati hadi unaonekana kero. Au basi akifanya anaharibu.
As a producer nimekuwapo na watu mbalimbali kwa kukutana au hata kuishi nao pia. Kiukweli, unakutana na mtu hadi unavutiwa naye vile anavyojielewa na kujitambua (Namaanisha kushirikiana katika harakati tu za maisha, mpwa usije ukaanza kunipoint). Kuna mtu mwingine yaani hata hutamani hata akusogelee.. Hata mimi naweza nikawa sijitambui ila unakuta mwingine ni high level.
Na kwa walio katika uhusiano. Mwanaume unamsichana ambaye yeye ni apate tu sex tosha. Hawezi hata kupika, kufua, n.k.
Show ikikwisha, kila mtu kwao! 😂
Yaani hadi majirani wakushangaa. Binti muda wote ameinama kwenye rununu. Cha ajabu jikoni kunaweza kukawa na kila kitu labda mboga ikosekane. Basi aulize vipi, tunapika nini? Lakini huyu unakuta tu ametulia anataka muende mkaninue chips mkule. Haya kuleni sasa! Na sijui mtafungiwa kwenye foronya au mtaenda na hotpot? 😂
Hapa sisemi tu kwa wapenzi. Hata wale ambao sio wapenzi. Umeenda kwa mtu, ulizia kama kuna uwezekano wa kufanya chochote kinachowezekana kwa wakati huo. Yeye ndio atakuambia kama ndio au hapana.
Uko na ndugu yako nyumbani kakutembelea (Ke), hawezi hata kuosha bakuli! 😁
Jamani tujitahidi kujiongeza, tusingojee hadi maelekezo. Uliza.
Na kuna wale watu ambao hawajitambui. Uchafu umetangulia mbele kama wa ndagu.
Kabla hujaingia ofisi za watu hakikisha hukeri. Sio unakera mpaka watu wanashindwa kukuhudumia. Mwisho wanakuambia hii huduma leo haipatikani. Umeingia na harufu za ajabu kama ulilala na mbuzi ama niaje! Viatu vimeambukiza miguu inanuka kama ulikuwa umechovya miguu kwenye mzoga. Halafu watu washindwe kukuhudumia, uanze kulalamika eti ooh wanajisikia, wanajiona. We mbona hujajiona kama unanuka? 😂
Hata kama ni mwanaume, umetoka kazini ukakuta kuna wageni, pitiliza kaoge ndio uje uongee na wageni. Sio unaenda kukaa na majasho yako unasababisha watu wanakohoa.
Haya, umezoea kwenda kwenye miji ya watu bila taarifa. Ama kila muda, kila saa, kila siku wewe nikuzurura tu kwenye miji ya watu. Jamani, watu wengine wanasiku za matambiko. Wape muda baasi wafanye mambo yao. Sio waanze kujiuliza, sijui leo atakuja, sijui hatakuja!! Unajua ndio hatuwezi kukufukiza, ila jiongeze basi. Unatembelea tembelea kwa kijana/binti hajaoa/hajaolewa. We unaenda enda tu. Je kama hiyo siku anatakiwa kuwa na uhuru kwa ajiri ya mtu wake?
Ngoja niishie hapa kwa siku ya leo, ila..!? Au basi!
Kwenye mitandao ya kijamii, nifuate as De Opera / @deoperacc






