Asante kwa kutembelea DoHub! 😊

Ikiwa umewahi kuguswa na kile tunachokifanya, tunakukaribisha kwa upole kabisa kuunga mkono jitihada zetu iwe kwa kuchangia kiasi chochote au hata kutangaza biashara yako kupitia jukwaa hili.

UMUHIMU NA FAIDA ZA KUJALI

Siraj Kingi
0

 

Habari za muda huu mpwa? Natumaini unaendelea vizuri na nimefurahi tumefanikiwa kukutana katika chapisho hili.

Mpwa kuna jambo leo nataka nikueleze ambalo ni la msingi sana katika maisha yetu hasa katika kudumisha uhusiano, urafiki na hata undugu. Pia katika kazi ni muhimu sana, nalo ni 'Kujali'.

Tukianzia katika uhusiano, suala la kujali hutengeneza nguvu kubwa sana katika uhusiano kwani huongeza uthamani mkubwa. Mfano, kujali kunaweza kuwa kwa mambo au namna tofauti. Mnaweza kuwa katika uhusiano na mkajuana vizuri yaani kila mmoja akamjua mwenzie kiuchumi, kihisia na kifikra. Kuna muda kinywa hakiwezi kuzungumza, ila mwili na matendo huashiria hitaji la kitu fulani.

Mwanaume hahitaji kusubiri aombwe hela ya matumizi, ila yeye kama mwenye kujali kama anao uwezo atafanya hivo. Kingine ni kwenye suala la muda. Maisha ya sasa ndio kiukweli ni magumu na kila mtu anajitahidi kupambana kadri ya uwezo wake, ila sasa tenga muda wa kuweza kuzungumza na mwenzio mpate kujuana vizuri. Kuna uhusiano unavunjika kwa sababu ya kutojaliana. Huyu yuko bize, hana muda hata wa kuzungumza na mwenzie. 

Tuachane na hilo la mahusiano twende kwenye suala tu la maisha ya kawaida, na hapa nitapin kwenye wafanyakazi iwe wa ndani au sehemu zingine.

Cha kwanza mimi kama mimi, nilishasema siwezi kukaa na mtu namuita 'Mfanyakazi'. Namtambulisha kwa watu eti huyu ni mfanyakazi wangu. Nitawaambia huyu ni ndugu yangu tunasaidiana kuhakikisha mambo yanaenda sawa. Sio unakuta mtu kashiba mchuzi wa supu na chapati kwa kutafuta sifa aonekane yeye ndiye bosi, anasema 'Huyu ni mfanyakazi wangu nimemuajiri kwenye kampuni yangu, yule aliyekuwepo alizingua nikamleta huyu kutoka Shinyanga'. Kiukweli hapo hata mfanyakazi hawezi kufanya kazi kwa moyo wala kutia juhudi katika kazi hiyo bali atatimiza wajibu tu. Ile kazi hawezi kuiona kama kazi yake.

Siri ya mafanikio ni kujali wenzio pia hata kama wewe upo katika nafasi gani.

Sio unatambulisha mfanyakazi wako, wewe umepiga suti, yeye sura imepauka kama mpembua simenti. Haki mimi hapana. Bora yeye avae suti, mie nivae tu kawaida coz hiyo ni afya ya akili pia.

Ngoja nikuibie siri. Ukitaka mfanyakazi wako wa ndani afanye kazi kwa kujituma na akufanyie kazi vizuri, onesha kumjali. Kama ni nguo, viatu, n.k mnunulie. Na hivo vitu ulivomnunulia usimkate kwenye mshahara. Jitahidi kuuvaa uhusika wake. Jiulize, kama mimi kuna muda nahitaji kitu fulani na yeye vile vile. Sio mnaishi kama vitani.

Kingine kama uko na mafundi wowote wale, fanya kuwahudumia ipaswavyo. Sio asubuhi hawajanywa hata chai wanasubiri cha mchana, nacho kinakuja tonge moja. Hapo utafeli, hawawezi kukufanyia kitu kwa umakini. Achana na maswala ya kula kwao, we wahudumie tu kama uwezo upo na Mungu atakubariki pia.

Hata katika wafanyakazi wa kwenye maduka. Wengi wanalalamikiwa wanaficha/wanaiba hela. Ni kweli lakini kwenye 100%, basi watakuwa asilimia 2%. Fanya kumuhudumia kama nilivokueleza hapo kwa mfanyakazi wa ndani uone kama atakuibia au kuficha hela. Kuna wengine wanakosa jinsi. Hawana pa kwenda, mshahara wenyewe kidogo matumizi nayo mengi, Bosi mwenyewe huna huruma kwanini asikuibie?

Hata kwa watoto pia, onesha kuwajali nao watakupenda kwa dhati. Tambua wanapenda nini na uwapatie. Watakumiss kila uwapo mbali nao.

Mpwa, mimi niishie hapo siku ya leo na ninadhidi kukumbusha kuwa suala la kujali ni muhimu sana kwa sababu unapomjali mtu yeye mwenyewe huongeza juhudi na umakini wa kukufanyia jambo lako.

Kwenye mitandao ya kijamii nifuate kupitia De Opera au @deoperacc.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Tafadhali Usitume Barua Taka Hapa. Maoni yote yanakaguliwa na Msimamizi.
Post a Comment (0)
 
 
Tovuti yetu hutumia vidakuzi kuboresha matumizi yako. Jifunze Zaidi
Accept !