Karibu tena katika makala hii.
Leo nitazungumza kuhusu mawasiliano. Jinsi ya kukuza, kujenga na kuimarisha.
Mawasiliano ni kitu muhimu sana katika maisha yetu. Mawasiliano yanaweza kukuinua kutoka hatua fulani, kuipima hekima/busara yako, au kutengeneza uaminifu kati ya mtu na mtu au kikundi.
Kuna aina mbili za mawasiliano:
- Mawasiliano ya Vifaa (Devices) — hususan simu
- Mawasiliano ya Kijamii (Social Communication)
Nianze na mawasiliano ya vifaa(simu).
Kuna baadhi ya watu huchukulia tu mawasiliano ya simu kama ni kitu cha kawaida tu na hayana maana sana.
Sasa, ngoja niseme! Mawasiliano ya simu yanaweza kukufanya uonekane wewe ni mtu mwenye hekima na busara sana kwa namna unavyoitumia. Mtu anaweza kukushusha hadhi na kukuondelea thamani endapo utatumia simu vibaya.
Mfano, ni namna mtu unavyoweza kumuuliza, kumjibu, kuzungumza.
Mtu anashushwa thamani au kupandishwa thamani wakati gani?.
Conversion ya Calls na Chats - Hapa ndipo wengi huonekana wazi.
Mara nyingi watu wenye ufahamu wa juu huweza kugundua kuwa huyu ni mtu makini au la.
Jinsi unavojibu(Replies), maswali, na mambo mengine. Huyu mtu utamfanya siku nyingine aendelee kuwasiliana na wewe ama asiwasiliane na wewe.
Kingine katika simu ni Uwajibikaji (Responsiveness).
Hapa ndio changamoto kubwa. Unaweza kumpigia mtu akawa katika mazingira ambayo si rahisi/ngumu kupokea. Baasi akili yako itaelewa kuwa mtu huyu atakuwa busy au simu kaweka mbali.
Sasa mtu huyu uliyemtafuta afanye nini ili usione kama ameidharau simu yako na siku nyingine uwasiliane naye bila wasiwasi.?
Kama mtu huyu alikuwa na access ya simu na anauwezo wa kujibu, basi atakujibu kwa lugha ya utulivu hata akisema “Samahani, siko kwenye mazingira mazuri sasa. Ntakupigia baadaye.”. Yaani atatumia maneno ambayo wewe mwenyewe yatakufanya ujisikie amani. Inaweza kuwa kwa kupokea au sms.
Au anaweza asi-respond kwa wakati huo, ila baadaye atakutafuta kukuomba radhi. Lakini hii huangukia kwa watu wenye uelewa, yaani haoni kama neno "Samahani" kwake ni almasi.
Kuna watu kusema samahani, pole, ni kama wanaweza kuuawa.
Mwingine ukimpigia simu na ana- access nayo lakini huitazama tu, na hata akiwa busy baadaye hawezi kukutafuta.
Au unaweza kumpigia akaikata ghafla kama imepitiwa radi 😀, pasipo kureply au basi akuambie changamoto. Unaweza waza huko aliko ametekwa.
Matumizi ya lugha nzuri kwa baadhi yanaweza kuwa changamoto pia. Unaweza mpigia akashindwa kupokea ila akakutumia ujumbe "Tuma message", "Unasemaje?", au "Sema shida"😀
Sasa, majibu haya sio soft na pengine ikatafsrika kuwa ni ya shari au aliyeituma hajapenda kupigiwa. kama aliyetumiwa ni mtu wa kunata sana huwezi kuijibu.
Wapo watu ambao ndio maisha yao. Kupokea simu ni msala. Na unakuta hana busy yoyote ya kufanya hivo.
Sasa, kwa namna hiyo unaweza ukajipata umepoteza mawasiliano na watu. Hata wakiwa na jambo muhimu au connection hawawezi kukutafuta. Lakini ukiwa na response nzuri ya mawasiliano itakuwa ni mwanga kwako.
Conversions/chats za ku-delay huwa zinapunguza/kuua mawasiliano.
Ukiwa busy, mwambie mtu kuwa samahani, hatutafanikiwa kusogoa sasa.
Na wewe unaetaka kusogoa, muulize kwanza kama yuko huru kabla hujaanza kumlaumu kuwa ana-load sana kwa jumbe zako.
Vilevile, kuna mtu ambaye akikupigia mara moja, huona haitoshi. Atakupigia simu yako mpaka atahakikisha inaisha chaji au ita-vibrate mpaka ihame ulipokuwa umeiweka na kama hukuiweka vizuri basi ujiandae kuweka kioo kipya.
Hii humfanya mtu akuone kama wewe si mtu unayefaa.
Simu ya afya ni moja tu unatulia, ukipita muda hajakutafuta, basi mtafute tena asipopokea muache. Kama ni mtu mwenye akili timamu atakutafuta.(Ila kama unamdai wewe piga tu mpaka akulipe!, na asipopokea tumia namba ngeni ambayo hana 😄) ... joke..
Kingine katika suala la mawasiliano ya simu, ni kuepuka kumpigia mtu simu ambazo hazina maana na hujajua mazingira yake yanaruhusu. Hii itamfanya awe anaikwepa simu yako, na utabaki ukimlaimu kwa kutoijali simu yako.
Unakuta mtu anakupigia kwa sababu dakika zake zinaenda kuisha muda wake.
Au mwingine anakupigia anaanza kukukumbusha ujunga wenu wa jana bila hata kujua mazingira uliyopo, mbaya zaidi 'earpiece speaker' ya simu yako ni kama umeweka Loud. Umeshusha volume lakini bado iko juu kila mtu anasikia. 😂
Sasa, ili mtu asikwepe simu yako, ni muhimu kuzingatia.
Ili mtu aendelee kuwasiliana nawe, ni muhimu kuzingatia.
Ukiwa busy, using'anga'nize kuongea au ku-chat kwa sababu utajikuta unamjibu mtu vitu shortcut kiasi cha kwamba utamfanya ajisikie vibaya na asiwasiliane nawe au kukushirikisha jambo muhimu wakati mwingine.
Kuna siku tulikuwa katika mipango tu ya harakati za maisha katika deal fulani. Nilikuwa mimi na jamaa yangu mmoja hivi. Sasa deal likawa linahitaji watu 3, ikabidi tusemezane kumpigia rafiki yetu mwingine ili naye aungane nasi. Yule jamaa yangu akasema 'Yule rafiki yetu kwenye mawasiliano ni changamoto. Huwa hapokei simu. Ni heri tutafute tu mwingine'. Tukatafuta mtu mwingine tuka-flash deal letu.
Bila shaka kupitia mfano huu umeona nguvu ya mawasiliano thabiti.
Haya, niende kwenye mawasiliano ya kijamii (Social communication).
Hii inafanya hata ukipita njiani kila mtu anatamani kuongea na wewe. Vile unarespond watu. Maswali na majibu unayowapatia. Inakupa nguvu katika jamii.
Katika mazungumzo, watu wanaweza kukushusha kwa njinsi unavyowajibu na wasitamani kuwasiliana na wewe.
Miadi ni jambo muhimu sana. Kuna watu wamejikuta wakijihisi vibaya ni kwa sababu wamepita njia ambazo si sahihi katika kujenga mawasiliano.
Mfano, unaenda kwa mtu ukihitaji kongea tu hadithi za kawaida bila hata kuuliza uwepo wa muda wake kuwa yuko huru?.
Unaenda unakuta yuko busy. Unamuongelesha anajibu kiufupi na wakati mwingine anakujibu vitu ambavyo hata yeye mwenyewe haelewi amekujibu nini. Ukimuuliza 'eti unasema?' yaani hakumbuki kabisa mara nyingi atakuambia urudie swali ulilokuwa umeuliza. Hii ni sababu akili yake yote iko kwenye kile anachokifanya, pengine kinahitaji utulivu wa hali ya juu, na kibaya zaidi wewe uliyemtembelea uwe ni mtu muongeaji sana na vitu unavyoongea havieleweki.
Hii itafanya mawasiliano yapungue/yaishe baina yake na wewe kiasi cha kwamba akikuona tu, anapata safari ya kutoka.
Mfano mwingine, umekuta mtu amekaa inaweza kuwa mahali fulani tulivu, ukamfuata na kuanza kumlazimisha muanze kupiga stori bila kuomba ruhusa. Matokeo yake anakuachia kiti. Na hapo wewe utajihisi vibaya na itakuwekea ki-chuki moyoni, ambapo hata siku nyingine mkionana, hakutokuwa na mawasiliano mazuri.
Unahitaji mawasiliano ya simu kutoka kwa mtu mliyeonana au kukutana mara ya kwanza. Kuna namna ya kutumia lugha vizuri. Ukitumia lugha vizuri huyo mtu hatakuwa na ugumu. Akikataa si lazima, ukilazimisha hata kama moyoni alitaka kukupatia, ataghairi kwa sababu wewe unakuwa kero tu kwa huo muda mfupi, vipi kwa muda mrefu?.
Mawasiliano ni kitu muhimu sana katika maisha yetu ya kila siku. Ndio hutufanya tuvuke katika hatua fulani.
Mawasiliano huleta umoja na kutengeneza msingi.
Mawasiliano kutengeneza amani, umoja na upendo.
Palipokosa mawasiliano, hakuna amani wala upendo.
Kama mko kwenye uhisiano/ndoa na hakuna mawasiliano mazuri basi migogoro haiishi, na mara nyingi hatma yake ni utengano.
Mimi naishia hapa mwana DoHub. Tukutane tena katika makala nyingine. Uwe na siku njema.
Makala hii imeandaliwa na Siraj Kingi (De Opera)






