Asante kwa kutembelea DoHub! 😊

Ikiwa umewahi kuguswa na kile tunachokifanya, tunakukaribisha kwa upole kabisa kuunga mkono jitihada zetu iwe kwa kuchangia kiasi chochote au hata kutangaza biashara yako kupitia jukwaa hili.

JINSI URAFIKI WA JINSIA MBILI TOFAUTI UNAVYOWEZA KUKWAMISHA MAMBO

Siraj Kingi
0

Habari za muda huu mpwa wangu? Natumaini unaendelea vizuri na tunakutana tena kwenye blog hii ya DOHub.

Leo nitaenda kuzungumza kuhusu urafiki kati ya jinsia mbili tofauti, jinsi unavyoweza kuharibu/kubomoa uhusiano uliokwisha jengwa au kuzuia/kukwamisha ujenzi wa uhusiano mpya.

Si jambo baya kujenga urafiki, lakini tazama urafiki unaokuwa nao unakupa faida ama hasara?.

Unakuta jinsia ya kiume yeye rafiki zake ni wasichana au wanawake pekee. Na hata yeye anasema kabisa rafiki zake wengi ni wa kike. Hata msichana vile vile, yeye rafiki zake ni wavulana au wanaume tu.

Mfano: Wewe ni wa kiume, una rafiki ambao au ambaye muda wote unakuwa naye, kila kitu unamuhusisha. Mnatoka, mnatembeleana yaani kama vile ni wapenzi lakini hata hayo mawazo hamna, hadi wakati mwingine watu wanaweza kuzungumza kuwa ninyi ni wapenzi kulingana na urafiki huo. 

Kama ni kijana hujaoa na unatafuta mchumba, sahau hilo kwa sababu wasichana wenye akili huhofia kuingia kwenye mashindano. Wanahisi wewe tayari unaye mtu/mpenzi. Unajikuta unaanza kulaumu kuwa una bahati mbaya. Kingine wanaona mnavyo-react. Mnavyoshikana mikono, pambaja n.k.

Kama mnafanya kazi ofisi moja, mazoea yanapitiliza. Ameketi kwenye kiti wewe unaenda kumkalia kwenye rapa/mapaja na watu wanaona kabisa. Unakumbatia kila msichana ukiita 'Ku-show Love'.

Kwa mwenendo huu, kama ulikuwa tayari unauhusiano, utavunjika. Kama ni ndoa, itavunjika. Labda uliyenaye roho yake ni ya kujaza kwa upepo ndio utakaa naye.

Hata kwa wasichana/wanawake. Binti hujaolewa, unaanza kutengeneza 'Urafikinaizesheniship'. Sahau kuchumbiwa. Mwanaume serious mwenye akili huwa hapendi kuingia kwenye mashindano.

Lazima utengeneze 'Stop touching me' kwenye mind yako. 

Vijana huwa hawarukii wasichana wanaojitambua na kujielewa. Ukiona wanakurukia rukia, keti utafakari. Umewafungulia mlango. Mwanaume/mvulana hachekewi. Ukimchekea umemuita. Kila atakayekutana na wewe atakushikashika, cha ajabu huwa hawatazami mazingira au uko na nani. 

Mwanamke aliye kwenye ndoa, kuendekeza hiyo ni mbaya sana. Utafanikiwa kama huyo mme umeukumbatia ubongo wake. Na hata hivo kuna mwisho.

Kwahiyo, hatuna budi kutengeneza mipaka. 

lazima utambue wewe ni nani. unaweza kuwa na thamani kubwa sana ila mazingira uliyokwisha yaandaa yakaimeza thamani yako na ukawa ni street ball.

kwa mvulana anaweza kuona tu ni sawa kwa sababu, umri wa mwanaume unavoendelea kuongezeka ndio huvutia zaidi, lakini kwa mwanamke umri unavoendelea kusonga mbele basi huwa ni kinyume ya mwanaume. hata wale rafiki zake wa kiume aliokuwa anamaliza nao muda wanaisha. 

Mimi naishia hapa siku ya leo mpwa wangu. uwe na siku njema.

Unaweza kunifuata katika mitandao ya kijamii kupitia Facebook De Opera .

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Tafadhali Usitume Barua Taka Hapa. Maoni yote yanakaguliwa na Msimamizi.
Post a Comment (0)
 
 
Tovuti yetu hutumia vidakuzi kuboresha matumizi yako. Jifunze Zaidi
Accept !