Watu wenye upeo, akili nyingi, na uwezo mkubwa wa kuona mambo na kutambua huwa wanaonekana ni wanaojisikia sana kwa sababu;
- Hawapendi watu wasiojielewa
- Hawavutiwi na watu wenye hulka za juu
- Ni wavivu kukaa na wavivu
- Hawapendi kona kona (Kuna namna hufikiria juu ya watu ambao huzungumza nao na kutambua kuwa "Haka kamtu ni kaongo kaongo, ni kahuni kahuni na kamwe siwezi kukasogeza karibu.)
- Huwa hawana maono na watu wasio na maono
- Huwa hawapendelei kuzoeana na watu wanaoigiza (Shammers)
- Huwa ni wenye msimamo thabiti
- Huwa wanaonekana ni wamejitenga kwa sababu hawapendi ujinga ujinga.
Kwa hiyo, kama umewahi kukutana na mtu wa namna hiyo zaidi ya mara moja na akakutupilia mbali, tambua kuwa unaweza kuwa mhanga katika orodha niliyoitaja.
Kuna namna mtu anaweza kuutetea udhaifu wake kwa kusema hakuna binadamu anaumba. Hii ni sawa na kutumia pesa ya akiba katika starehe huku ukisema "Maisha yenyewe ndio haya haya".
Mungu hakukaa kukuumba uwe dhaifu, bali ni matokeo tu ya kibinadamu, ila kuna udhaifu unaozalishwa na homoni ya ulimbukeni.
:Hatuna budi kuwa makini hasa ambapo tunazungumza mbele ya/ kuwadanganya watu wenye upeo kwani ndio wakati wa kuishusha thamani ambayo mtu huyo amekupatia.
(Mungu haji moja kwa moja kukuambia uache pombe, bali kuna mtu tu anaweza tokea akakuambia hivo. Mungu anatumia watu).






