Asante kwa kutembelea DoHub! 😊

Ikiwa umewahi kuguswa na kile tunachokifanya, tunakukaribisha kwa upole kabisa kuunga mkono jitihada zetu iwe kwa kuchangia kiasi chochote au hata kutangaza biashara yako kupitia jukwaa hili.

BAADHI YA WANAWAKE WA KIAFRIKA, TABIA KATIKA UMRI TOFAUTI.

Siraj Kingi
0

 


Hujambo mpwa? Natumaini unaendelea vizuri. Karibu tena katika jukwaa hili na leo nitaenda kuweka bayana mambo kadhaa ambayo nimefanya utafiti na kugudua 80%  ya tabia/mienendo za mwanamke wa kiafrika katika hatua/umri tofauti tofauti.

Ninaomba radhi kwa chapisho hili kwani, kuleta mapokeo tofauti na kuweza kulichukia au kumchukia mwandishi wa chapisho hili. Lakini tupo katika kuelimishana na kujifunza. Waswahili tunasema "Usimtende akuamshae".

1: Katika umri wa miaka 14, Huanza kuonekana ni mabinti wa kuanza kutamanisha kwa uzuri/Mvuto.

2: katika umri wa miaka 16 huanza kujiskia na kujiona wanatamani kua na wanaume waliowapita umri,na hutamani kua na wale wanaume wenye kuvutia hasa katika mazingira yaliyowazunguka, mfano shuleni,au kwenye makundi yao.

Huvutiwa vutiwa na wale wanaowatazama kwenye tamthilia, telenovela. 

3:Katika umri wa miaka 18 wengine kwao inaweza kua ndio huanza kujaribu ngono kwa mara ya kwanza. Ataanza kumsifia huyo mwanaume, na kuweka mipango ni jinsi gani hatakaa amsaliti huyo mwanaume. Huweka ahadi kemkem kwamba huyo ndiyo mwanaume wa maisha yake.

4: Katika umri wa miaka 20, anaweza akawa ndio ameingia chuo sasa na huko ataanza mahusiano mapya, na taratibu ataanza kupunguza mazoea na yule mwanaume wake wa awali na taratibu anaanza kuvisahau vile vi ahadi vyake vya uongo na kweli. 

5: Katika umri wa miaka 22, Hapa anaanza kutengeneza mazoea na urafiki na mabinti ambao hupenda kuvaa nguo za gharama, kumiliki vitu kama simu ambazo ziko nje ya uwezo wao, pia ni mabinti ambao shabaha zao ni kutembea ama kuonekana na wanaume wa gharama. Anaanza kuishi kwa kushindana ama kutaka kujulikana nayeye yumo. 

6: Katika umri wa miaka 24, Ameshakua wa gharama sasa anatembea na wanaume wenye uwezo fulani kifedha, hata maprofesa hivyo huu wakati kijana wa kawaida tu choka choka fulani hivi hata ukiomba namba, utapewa jibu ambalo unaweza ukalaani babu zako kwanini hawakuwaga matajiri.

7: katika umri huu wa miaka 26, starehe zimepamba na chart yake imepanda yuko kwenye peak,au prime.

Anaanza kupandisha viwango tu kwa wanaume. Kwanza anakua anataka mwanaume mwenye uwezo mkubwa, sifa, cheo na pesa tu.

8:Kwenye umri wa miaka 26-27, Kichwa inaanza kukamata chaneli (Akili inachaji). Ile chaneli ya huruma na nidhamu baada ya kuona matokeo hasi kutoka kwake ama rafiki zake. Katika umri huu anaanza kuyahofia kila mahusiano, akiingia anachomoka haraka kila baada ya kutokuelewana na mwenziye, anaamini anatafunwa tu kama pizza ama chocolate, huku akihisi kuwa mtu muda wowote anaweza kumkacha.

9: kwenye miaka 28, wale wanaume wote waliokua wakimsifia na kumpamba na wengine waliokua wakimweleza ni jinsi gani wanampenda,sasa wanamshusha standards. Wanafungua vioo, wanamuona, wanamtumia, wanarina asali kwa hasira na kuishia zao.

Anaamua kurudi kwa Ex wake na huko nako anakuta kambi ilishapata mkimbizi. Kila chaka lina nyoka.

10: katika miaka 29, Hakuna hata mwanaume mmoja kati yao anayemchumbia.

11: katika miaka 30, mikesha ya maombi ya mabwana, Makusanyiko ya kipentekoste, maombi ya komboa tumbo, makongamano ya kanyaga mafuta, makusanyiko ya vuka na chako.

Akija kwa manabii anaambiwa lete chupi tuombee, na mbaya zaidi kwa manabii uchwara uchwara akilegeza nyuzi tu nabii anamtumia nayeye.

12: Katika miaka 32-35, Ni kuhama kanisa baada ya kanisa, msingi baada ya msingi, baba niombee baba niombee. Wanaanza kua watumwa tena wa dini, Na akili zinakua utupu unaojazwa kila kitu na kuamini pokea.

13:Katika miaka 40, Anaanza kuona na kuamini ndugu zake wa kifamilia na ukoo ni wachawi ndio wanaomchawia. Anaona wengine ni wachawi, washirikina, na washirika wa falme za giza. Kumbe yeye ndiye kajichawia mapema tu.

14: Miaka 45, Anakua ni mshirika wa kudumu wa taasisi fulani ya dini. Ni mshirika anayeongoza kwa kulia usiku na mchana hapo kanisani.

15: Miaka 50, Huyu sasa ni kungwi na motivational speaker. Anaanza wafundisha mabinti ujinga wake. Anaanza kuwa kungwi anayepanda mbegu za chuki kwa masingo mama. Anaanza kuwajaza mabinti namna ya kuishi bila mwanaume wakati yeye alihangaika miaka 20 yote katika kutafuta suluhu ya mbegu aliyoipanda ujanani.

HITIMISHO

Binti jitunze asili itakutunza.

Binti jiheshimu asili itakuheshimisha

Binti Upendo wa kweli ni mara moja.

Binti mwanaume kukosa hela, usimtafsiri kichwani mwako kwamba huyo ni masikini kukosa pesa sio umaskini bali ni hali ya mpito ila tu umaskini ni tatizo la akili.

Mimi natamatisha hapa mpya wangu. Wiki ijayo nitazungumza kuhusu tabia chafu na mbaya za wanaume ambao hawajielewi wala kujitambua. Kazi yao ni kuharibu/kuvuruga maisha ya binti/wanawake. Mwanaume kama unaona huwezi ishi na binti wa watu, usimuharibie maisha. Kuomba omba namba kila binti/mwanamke kama vile unataka uwaajiri.

Ahsante sana! ^deoperacc

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Tafadhali Usitume Barua Taka Hapa. Maoni yote yanakaguliwa na Msimamizi.
Post a Comment (0)
 
 
Tovuti yetu hutumia vidakuzi kuboresha matumizi yako. Jifunze Zaidi
Accept !