Kila mtu anaroho nzuri ila kuna hii kitu "Huruma".
Yeyote mwenye huruma/anayeguswa na jambo fulani ndio amezoeleka kama "Mwenye roho nzuri".
Yule asiye na huruma/mkatili/mbinafsi ndiye amezoeleka kama "Mwenye roho mbaya".
Kwa namna fulani ya haraka haraka, watu wenye huruma ni wachache wanaofanikiwa kwa sababu, kwanza huwa ni watu ambao wapo kwenye vita kubwa kwa sababu ya kujitoa kwao. Pili huwa wanatoa chote walichonacho kumpa mtu aleyehitaji. Hata kama akiwa nacho kidogo, lazima tu atatoa kwa sababu ya huruma.
Akiibiwa au kudhulumiwa hawezi kwenda polisi.
Huwa hawezi kuingia kwenye mapambano/vita kugombania kitu ambacho anauwezo/uhakika wa kukitafuta.
Watu wenye huruma wapo kila mahali, mfano unaweza kwenda kwenye ofisi fulani ukakuta watoa huduma wawili, miongoni mwao anaweza kuwapo yule mkatili na mwingine anaweza kuwa ni mtu mwenye huruma ya aina yake. Katika huduma unayohitaji ukapokelewa na yule mkatili mwenye short words na kulingana na sisi binadamu hatulingani akili basi unaweza shindwa kumuelewa vizuri kulingana anavoyakandamiza na kuyakaza maelezo mwisho mnatofautiana. Yule mwenye huruma atatamani akutafute akusaidie na muda mwingine anaweza kukuomba hata mawasiliano yako kama mazingira yanaruhu. Basi atajitahidi hata ajifanye anatoka nje ili akungojee. Ni kwa sababu tu ya huruma na alivyoguswa na changamoto yako na anaona hilo anaweza kulitatua.
Kulingana na jambo atakalolifanya la kukusaidia, anaweza onekana mtu mbaya na mnafiki kitu ambacho kinaweza tengeneza vita baina yake na yule mtoa huduma mwenza. Atafanyiwa figisu hadi afukuzwe kazi. So hatokuwa na kazi tena. Hapa nakumbuka msemo wa "Wema umeniponza". Na hapa lazima maisha yasimame.
Kiukweli, kama ulizaliwa tayari ni mwenye huruma basi hata ukifanya nini, kamwe huwezi kujifunza kuwa mkatili. Kuna muda unaweza kujifanya mwenye roho mbaya ila utahisi nafsi inakusuta na kukwambia acha upuuzi, hujazaliwa hivo wewe. 😄
Kuna mtu anaweza kuwa amekukosea na ukamtamani na kumngojea kwa hamu kwamba fulani leo nitamuonyesha. Basi akishakuja walaa hata huna habari naye. 😂 Ndio kwanza mnafurahi na kucheka na unapitishia kahasira kako humo humo na kumwambia ujue wewe jamaa yangu sometimes unazingua. 😂
Sasa katika mafanikio, ukiwa na huruma ni mara chache sana kufanikiwa kwa haraka. Kila jambo ambalo unalifanya la kukupa maendeleo utakuwa ukihisi unaonea mtu mwingine. Ukipata Behind the Scenes hata huwezi thubutu kushiriki. 😂
Niseme tu hofu ya Mungu imetawala kwenye kipengele hiki.
Ila kumbuka, huruma na wema ni hazina. Ukifanya wema leo hutayaona matokeo leo, bali yanaweza tokea katika kizazi chako. Mtu uliyemsaidia leo anaweza saidia kizazi chako baadaye, au kizazi cha uliyemsaidia leo kikakusaidia wewe au kizazi kwa kizazi vikasaidizana.
Mimi naishia hapo. Nakuacha na wimbo huu kutoka kwa Jennifer Mgendi akikuambia "Wema ni akiba".
Usiache kunifuata katika social platforms kupitia @deoperacc. Bonyeza hapa kunifuata Twitter






