Habari wapwa!
Natumaini haujambo, pole kwa majukumu ya kila siku.
Leo nagusia kuhusiana na jambo ambalo kiukweli limezoeleka kabisa wala sio geni hapa mjini.
Kuna baadhi ya watu tumekuwa tukidharau vitu/mambo/watu hii ni kwa sababu tu tunataka tufanye vitu kutokana na matamanio au matakwa yetu. Tunataka tupate matokeo chanya kutokana na nini sisi tunataka na kupuuza kwa kuona vitu vingine havifai na haviwezi kutufikisha mahali tunakotaka. Iwe katika biashara au maisha tu ya kawaida.
Hivi unajua unajua baraka akupazo Mungu zimejificha wapi?
Sasa ngoja nikuibie siri!
Baraka zipo kwa vitu tunavyovidharau, baraka zipo kwa watu tunaowadharau na hazipo katika matamanio yetu ndio maana wakati mwingine unaweza kufanya jambo likakamilika lakini likakosa matokeo mazuri.
Kama kuna jambo lilikuja mbele yako lilikuja na kulidharau kaa chini na roho yako mjutie kwa kulikosa jambo hilo pengine ilikuwa ni baraka.
Mfano, kuna kijana mmoja alikuwa amesimama barabarani akisubiri usafiri kwenda mjini kutafuta kazi, mara akatokea mwehu. Yule mwehu akamwambia yule kijana 'Mimi nina makampuni mengi sana, ninauwezo wa kumuajiri yeyote hata wewe, nifuate ule maisha wewe'.
Yule kijana alimuangalia yule mwehu na kusogea hatua pembeni kidogo na kujisemea 'hili li chizi liniajiri mimi kwenda kula masalia jaani hahah'.
Baasi yule kijana alipata usafiri akaenda mjini. Alipofika mjini akatafuta kazi na hakufanikiwa.
Alifanya hivo hivo na siku zingine pia mwisho akakata tamaa.
Akaamua aingie mtaani na kuwa 'Gambling Boy' yaani kijana mcheza kamari. Pia alianza kutumia madawa ya kulevya na akawa kibaka.
Siku moja mida ya saa moja usiku akiwa katika harakati zake za kazi aliyoamua kuianzisha(ukabaji), akamkaba mwanamke mmoja na kumpora mkoba na simu.
Yule mama akapiga nduru watu wakaanza kumkimbiza yule kijana akakamatwa na kupelekwa polisi.
Yule mama akaenda nyumbani na kumweleza mmewe kilichotukia.
Yule mwanaume asubuhi akaenda polisi ili kumuona huyo kibaka ambaye alitaka kupora vitu vya mkewe.
Duh, macho kwa macho, uso kwa uso.. yule mwanaume akakutana na yule kijana.
Back days walisha wahi kukutana, huyu akiwa chizi, huyu akiwa kijana smart. Ila kijana smart aliona chizi hana lolote..
Baasi wakakumbushana, yule kijana akaomba msamaha. Yule mwanaume akamsamehe kisha akamtoa pale polisi na akamchukua wakaenda pamoja nyumbani kwa yule mwanaume. Yule kijana akaajiriwa na yule mwanaume na baadaye muda wa kuoa ulipofika akaozeshwa na maisha yakaendelea.
Hivi ulishawahikujutia kwa kile ulichokidharau?
Au hata sasa bado unajutia? Iambie tu nafsi yako kwamba kiukweli najutia.
Mambo kama hayo yanatufanya tusisonge mbele kwa sababu sisi tumekuwa ni watu wa kudharau.
Katika biashara, mtu anaweza akadharau biashara/kazi fulani kwa sababu ni ya kiwango cha chini anaona itamdharirisha hapa mjini, kumbe safari yake ya maisha ilipangwa ianzie hapo.
Katika uhusiano/uchumba, mtu anaweza akadharau mtu fulani kwa sababu ni wa kiwango cha chini anaona atamdharirisha hapa mjini, kumbe safari yake ya maisha ilipangwa ianzie hapo.
Katika maisha ya kawaida, mtu anaweza akamdharau mwenzie kwa sababu hana maisha ni maskini hana msaada wowote na anaona bora ajenge urafiki mtu mwenye hali nzuri kimaisha kumbe safari yake ya maisha ilipangwa wakutane na huyo maskini wafanye biashara pamoja ili wafanikiwe.
Kiukweli tunapishana na gari la mshahara!
Naitia yangu nukta hapa, ninaimani hujatoka kapa,
umezoa funzo si haba, na umejaza kunamo jaba.
tukutane next time. Mimi ni De Opera, kwenye mitandao ya kujamii unaweza ukanifuata kupitia De Opera au deoperacc
Uwe na siku njema!






