Asante kwa kutembelea DoHub! 😊

Ikiwa umewahi kuguswa na kile tunachokifanya, tunakukaribisha kwa upole kabisa kuunga mkono jitihada zetu iwe kwa kuchangia kiasi chochote au hata kutangaza biashara yako kupitia jukwaa hili.

UJUMBE WA LEO: KILA MTU AMEPEWA MUDA WAKE KATIKA MAISHA NA DUNIA HII

Siraj Kingi
0

Kila mtu alipewa/amepewa muda wake katika maisha na dunia hii. Usilaumu watu kwa kuona wako bize na muda wao.

Kubali tu kwamba wakati wa muda wako, ulianguka hukuutumia vizuri.

Kila mtu amepewa muda wake hapa duniani. Kuna kipindi cha kujifunza, kipindi cha kujenga, kipindi cha kuvuna na kipindi cha kupumzika. Hakuna anayeweza kuishi vipindi vya mwingine; kila mmoja hupitia safari yake kwa wakati wake.

Ndiyo maana si vema kumlaumu na kumhukumu mtu kwa sababu unaona yuko bize na muda wake. Huenda anapambana kujenga maisha ambayo kesho yatabeba yake na  watu wengi pia. Huenda anajaribu kurekebisha mambo ambayo hakuwahi kuyapata. Huenda anatumia muda wake kwa namna ambayo yeye anaona ni muhimu katika hatua aliyopo.

Mara nyingi tunapokosa muda wa mtu, huwa ni rahisi kudhani ametusahau au amebadilika. Lakini si kila umbali ni ishara ya kutokujali. Wakati mwingine ni matokeo ya majukumu ambayo maisha yameweka mbele yake.

Muda unaopita haurudi. Lakini kila siku mpya hutupa nafasi ya kutumia vizuri muda uliobaki. Pengine hiyo ndiyo zawadi kubwa ambayo maisha hutupa.

Jambo muhimu ni kuwa; kama upo kwenye muda jiulize 'Ninautumia muda vizuri?', na kama muda umeshakutupa, shika vizuri moyo pasipo kuwalaumu watu. Jiulize 'Je, nilipokuwa na muda, niliutumia vizuri?'.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Tafadhali Usitume Barua Taka Hapa. Maoni yote yanakaguliwa na Msimamizi.
Post a Comment (0)
 
 
Tovuti yetu hutumia vidakuzi kuboresha matumizi yako. Jifunze Zaidi
Accept !